JUMANNE, NOVEMBA 25
*TAJI YA UZIMA*
*_Baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake. — 2 Timotheo 4:8_*
📝 Paulo alidumu kuitazama taji ya uzima ambayo angepewa, si yeye tu ambaye angepewa bali pia kwa wale wote waliopenda kuonekana kwa Kristo. Lakini ni ushindi kupitia kwa Yesu Kristo uliomfanya kuwa na shauku kubwa ya taji ya uzima. Yesu asingetaka sisi tuwe na shauku ya kupata thawabu, bali anataka tuwe na shauku ya kufanya mapenzi ya Mungu kwa sababu ni mapenzi Yake pia, bila kujali thawabu tutakayopokea.
📝 Kipawa cha Mungu ni uzima wa milele. Bwana anatamani wote wanaoipokea neema Yake kumtumaini kikamilifu. Anatuita kudhihirisha imani safi na sahili, kumtumaini Yeye bila kuhoji juu ya kile tutakachopokea kama fidia. Tunapaswa kufanya kazi kwa moyo katika huduma Yake, tukionesha kuwa na tumaini thabiti kwamba atahukumu kwa haki.
📝 Katika maelezo ya mandhari ya hukumu, pale watakatifu watakapopewa thawabu, na hukumu kutolewa kwa waovu, watakatifu wanaoneshwa wakishangaa na kujiuliza ni nini walichokifanya kinachowastahilisha kupokea thawabu. Lakini walidumisha imani yao katika Kristo. Walikuwa wamejazwa na Roho Wake, na pasipo juhudi za makusudi, walimtendea Kristo, kupitia kwa watakatifu Wake, zile huduma zinazosababisha kupewe thawabu ya hakika. Lakini nia iliyowafanya kutenda hivyo haikuwa kutaka kupokea fidia. Waliichukulia kuwa ni heshima kubwa kukubaliwa kufanya kazi kama aliyofanya Kristo. Walifanya na walitenda sababu ya upendo waliokuwa nao kwa Kristo na wanadamu wenzao na Yeye aliyejihusianisha na jamii ya wanadamu inayoteseka aliyatambua matendo haya ya huruma na upendo kama aliyotendewa Yeye mwenyewe. Kila karama yetu na kila talanta yetu, tunawiwa na Bwana. Kila ushindi tupatao wote tunaupata kwa sababu ya neema Yake. Hivyo, hatupaswi kabisa kujivuna.
📝 Ikiwa tungeweza kukumbuka kuwa mbele ya ulimwengu wa kimbingu tuko katika kupimwa na kujaribiwa, kwamba Mungu anatupima, ili kuona tu wa roho gani, kungekuwa na tafakari ya kina na kuomba kwa bidii zaidi. Wale wafanyao kazi kwa usahili wanatambua kwamba mwanadamu peke yake hawezi kufanya jambo lolote jema. Wamejaa Shukrani na kushukuru kwa fadhila ya kuwa na ushirika pamoja na Mungu. Huduma yao imefungamanishwa na kanuni inayofanya zawadi na sadaka zao kuwa manukato mazuri. Wana ujasiri na imani ile ile kwa Mungu ambayo mtoto huwa nayo kwa baba yake wa kidunia.
📘 *Thawabu yetu si hasa kwa sababu ya kazi au jitihada zetu, bali ni kwa sababu ya wema, rehema na upendo wetu tulivyochanganya na matendo yetu kwa wale wanaougua, wale wanaoonewa na kuteswa (The Signs of the Times, Agosti 9, 1899).*
BASI NINYI NANYI KESHENI MAANA HAMJUI SIKU WALA SAA.
*MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI SANA*
0 Comments