Advertisement

MAHUSIANO

 


Mimi ni binti umri wangu ni miaka 25, sijaolewa bado dada yangu.


Kipindi nakaa Kwa dada yangu nilipata mchumba mpaka nikampeleka kumtambulisha Kwa dada, ila huwezi amini badae nilikuja kugundua dada kanizunguka ameanza kutembea na mchumba wangu, 


Iko hivi, baada ya Mimi kumtambulisha mchumba wangu ilipita kama mwezi tu nikaona mchumba wangu kabadilika sana, akawa hanitafuti, na Kila nikimtafuta anadai Yuko busy, Yani nikawa mpaka simuelewi, nikaanza kumshirikisha dada yangu lakini dada yangu alicho kuwa akinishauri ni kuwa niachane naye, kweli badae nilikuja nikaona Bora niachane naye japo niliumia sana.


Ilipita kama miezi miwili, siku Moja nilikuwa nafua nje nikawa nimeishiwa sabuni ikabidi niingie ndani, nilivyo fika ndani nikakuta simu ya dada mezani inaita, kuangalia namba ni ya yule mchumba wangu ila haijaseviwa, nikashangaa, ikabidi nisubiri simu ikate nikaichukua nikaanza kuangalia meseji na calls, nilikuja kukutana na mshangao mkubwa upande wa WhatsApp, Kwa kifupi ni kwamba dada alikuwa na mahusiano na mchumba wangu miezi mitatu tayari.


Ilibidi nifanye uchunguzi ndo siku Moja dada nikamfumania Yuko Kwa mchumba wangu ilikuwa siku ya jumapili, yeye alisema Hajisikii kwenda kanisani hivyo atatupeleka kanisani ila yeye atarudi nyumbani kupumzika, 


Alivyo tufikisha kanisani akawa amerudi nyumbani, na Mimi nikachukua boda nikarudi nyumbani, ila sikumkuta nikakuta tu gari imepaki ila yeye hayupo, ikabidi niende nyumbani Kwa mchumba wangu nikakuta mlango umefungwa Kwa ndani, nikagonga Kwa muda akawa amefungua mchumba wangu nikamsukuma nikawa nimepata upenyo nikaingia ndani ndo nikamkuta dada amekaa sebuleni, Dada alishituka sana akaanza na kulia akaniomba nimtunzie hiyo Siri.


Toka siku hiyo niliamua nikajitegemee sikumwambia mtu yeyote hicho kitu mpaka Leo, Yani imepita miezi nane toka hicho kitu kitokee lakini nimeamua kumtunzia hiyo Siri dada yangu japo moyoni bado Nina kidonda.


Sasa dada yangu mume wa dada ame endelea kunisumbua kunihitani kimapenzi, na alianza kunitongoza kipindi bado naishi kwao lakini nilikuwa namkatalia , nafsi yangu inatamani kumkubalia Kwa Sasa Ili kulipiza kisasi Kwa dada yangu ila nafsi nyingine inakataa, ijumaa pili iliyo pita aliishia kunivua nguo zote ila nikaja kubadilika nikamkatalia, hivi dada hapa nifanyeje Yani natamani kumlipizia kisasi dada yangu ila Sasa Kila nikitaka iwe hivyo mara nafsi nyingine inakataa haraka sana.

Post a Comment

0 Comments