Advertisement

NJIA ZA KUELEKEA MAISHA MAZURI

 




Wakazi katika makazi yasiyo rasmi katikati ya miji barani Afrika wanajulikana kuwa wanapitia mateso yasiyolingana yanayotokana na mazingira ya kutokuwepo usawa wa kijamii na kiuchumi na mara nyingi hutengwa na maono ya viwango vikubwa na sera ambazo zinatafuta kuifanya miji izidi kuwa salama na yenye ustawi (Birkmann, 2007; da Silva & Braulio, 2014; Dodman et al., 2013). 

Mvutano huu unadhoofisha uhalali wa ‘maono yanayoongozwa na utaalamu’, sera na hatua za kupima ustawi ambazo ziko mbali na uzoefu wa maisha ya wakazi wanyonge wa mijini. Kwa kuzingatia kazi mpya iliyojaribiwa pamoja na jamii katika makazi matatu yasiyo rasmi Jijini Dar es Salaam, nchni Tanzania, makala hii inatoa hoja kwamba mitazamo ya mbinu mpya na njia za nadharia za kushirikiana katika kuzalisha muktadha wa sera maalum kuhusu maarifa ya njia za kuelekea ustawi (inayotafsiriwa na jamii kama maisha bora, ‘the good life’ inaanzisha nafasi jumuishi kwa ushiriki wa jamii katika michakato ya uzalishaji wa maarifa ya mijini na uchunguzi muhimu wa kijamii unaoweza kuelekea ujenzi wa nadharia imara. 

Kwa kushirikiana na kuzalisha mbinu inayokubalika na kufaa katika uchunguzi huu na baadaye uandaaji wa nyaraka na uchambuzi wake, kazi hii inachangia manufaa ya majaribio katika uelewa wa kina kuhusu uwezo na vipaji vya jamii wenyeji kuunda na kushawishi utungaji wa sera za mijini na kwa njia hii utafiti unathibitisha kaulimbiu ya dunia-miji (Ong, 2011; Robinson, 2016) ambayo inaleta sauti mbali mbali na jiografia tofauti katika nadharia ya mijini katika kuzingatia zaidi tofauti ya uzoefu na michakato inayopatikana katika miji ya karne ya ishirini na moja. MANENO MSINGI Afrika; ubunifu katika jamii; Dar es Salaam; makazi yasiyo rasmi; ushirikiano wa kuzalisha maarifa; ustawi; kutokuwepo usawa wa jamii na uchumi; Tanzania. SUALA Makala hii ni sehemu ya suala la “Miji Jumuishi --Nafasi ya Haki” Cities of Inclusion-Spaces of Justince iliyohaririwa na Anja Nygren (Chuo Kikuu cha Helsinki, Ufini) na Florencia Quesada (Chuo Kikuu cha Helsinki, Ufini). © 2020 na waandishi; Mwenye leseni Cogitatio (Lisbon, Ureno). Makala hii imepewa leseni chini ya Creative Commons Attribution 4.0 Leseni ya Kimataifa (CC BY). 

Post a Comment

0 Comments