Advertisement

KUHANI MKUU



*KUHANI WETU MKUU MWAMINIFU NA MWENYE REHEMA*


*_✍️Wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele. — Waebrania 9:12._*


Akiwa kama mbeba dhambi, kuhani na mwakilishi wa mwanadamu mbele za Mungu, aliingia katika maisha ya wanadamu, akachukua mwili na damu yetu. Uhai kwa yule aliyehai, ni mkondo muhimu wa damu, damu ambayo ilitolewa kwa ajili ya uhai wa ulimwengu. Kristo alifanya upatanisho kamili, akiutoa uhai wake kama fidia kwa ajili yetu. Alizaliwa akiwa hana doa la dhambi, lakini alikuja ulimwenguni kwa jinsi ileile ya familia ya wanadamu. Hakuwa tu na umbo la kibinadamu, lakini alichukua asili ya mwanadamu na kushiriki katika maisha ya kibinadamu...


Yesu Kristo alivua vazi Lake la Kifalme, taji Yake ya kifalme na kuuvika Uungu Wake ubinadamu, ili kuwa mbadala na dhamana kwa mwanadamu, ili kwa kufa kibinadamu kupitia kifo Chake aweze kumharibu yule aliye na mamlaka juu ya kifo. Asingeweza kufanya hivi akiwa Mungu, lakini kwa kuja kama mwanadamu Kristo aliweza kufa. Kupitia mauti aliishinda mauti. Kifo cha Kristo kilimwangamiza yule ambaye alikuwa na nguvu juu ya kifo na kufungua milango ya kaburi kwa wote wampokeao Yeye kama mwokozi wao binafsi.


Kristo alitangaza juu ya kaburi lililokodiwa la Yusufu "Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima." Yeye Mkombozi wa ulimwengu, alimponda nyoka kichwa na kumnyang'anya uwezo wote wa kumfanya mwanadamu kuhisi uchungu wa nge; maana ameweka bayana uhai na hali ya kutokufa. Malango ya uzima wa milele yamewekwa wazi kwa wote wanaomwamini Yesu Kristo... Kwa kifo Chake, Yesu amefanya isiwezekane kwa wale wanaomwamini Yeye kufa milele...


Kristo aliishi na kufa kama mwanadamu, ili aweze kuwa Mungu kwa makundi yote mawili, wenye uhai na waliokufa. Alifanya hivyo ili kufanya isiwezekane kwa wanadamu kupoteza uzima wa milele ikiwa watamwamini Yeye. Uhai wa wanaume na wanawake una thamani kubwa machoni pa Mungu; kwani Kristo ameununua uhai huo kwa kuuawa badala yao. Hivyo akafanya iwezekane kwetu sisi kufikia hali ya kutokufa.


*_✍️Ndani ya Kristo Uungu na ubinadamu viliungana - Muumbaji na kiumbe. Asili ya Mungu, ambaye sheria Yake ilikuwa imevunjwa na asili ya Adamu, mvunja sheria, vilikutana ndani ya Yesu - Mwana wa Mungu na Mwana wa mwanadamu. Na kwa kuwa Yeye alilipa gharama ya wokovu kupitia damu Yake Mwenyewe, akiwa amepitia uzoefu wote anaoupitia mwanadamu, akiwa ameyashinda majaribu alipokuwa mbadala wa mwanadamu, akiwa, japo Yeye hakuwa na dhambi, amebeba aibu, hatia na mzigo wa dhambi, anakuwa mtetezi wa mwanadamu na mwombezi. Uhakikisho wa pekee ulioje, kwa nafsi inayojaribiwa na kuteseka, uhakikisho wa pekee kiasi gani kwa ulimwengu unaoshuhudia kuwa Kristo atakuwa "kuhani mkuu mwenye rehema na mwaminifu"! (The S. D. A. Bible Commentary, Ellen G. White comments, vol. 7, 925, 926)._*


*_MUNGU NA AKUBARIKI🙏._*

Post a Comment

0 Comments